• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na nchi za kiarabu wafungua ukurasa mpya

  (GMT+08:00) 2018-07-11 07:29:02

  Kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wenye ushirikiano kamili, maendeleo ya pamoja na kuangalia siku za baadaye kati ya China na nchi za kiarabu, ni jambo la kihistoria linalofungua ukurasa mpya kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili.

  Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipokutana na waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenzake wa Saudi Arabia Bw. Adel al-Jueir na katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Ahmad Abdoul Gheit kando ya mkutano wa 8 wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu unaoendelea hapa Beijing. Bw. Wang amesema China na nchi za kiarabu zimesaini nyaraka tatu muhimu kuhusu uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande hizo mbili, kutaja hatua mpya za kuimarisha ushirikiano wao katika sekta za uchumi na biashara, viwanda, nishati na utamaduni, na kuhimiza ushirikiano katika kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Ameongeza kuwa katika mkutano huo, China imeahidi kuendelea kulinda utulivu wa Mashariki ya Kati, kuunga mkono kithabiti juhudi za nchi za kiarabu za kulinda maslahi yao halali, na kuhimiza suala la Palestina kutatuliwa kwa haki haraka iwezekanavyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako