• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaahidi kupinga "vita ya kiuchumi" ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-07-11 08:52:51

    Makamu wa kwanza wa rais wa Iran Bw. Eshaq Jahangiri ameahidi kuwa Iran itapinga vikwazo vya Marekani vinavyoweza kuanza kutekelezwa katika miezi ijayo. Bw. Jahangiri amesema watakabiliwa na hali mpya na ngumu kutokana na vita ya kiuchumi itakayoanzishwa na maadui, na Iran itapinga vita hiyo kwa nguvu zote. Amesema Marekani, Israel na Saudi Arabia zinatafuta kutoa shinikizo la kiuchumi kwa watu wa Iran ili kufikia malengo yao, na ametoa wito kwa serikali kutumia mbinu mwafaka kukabiliana na njama zao. Kabla ya hapo rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuiwekea Iran "vikwazo vikali zaidi katika historia" endapo haitabadilisha mienendo yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako