• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump aendelea kukosoa washirika wa Ulaya kabla ya mkutano wa kilele wa NATO

    (GMT+08:00) 2018-07-11 08:53:10

    Rais Donald Trump wa Marekani ameendelea kukosoa washirika wa Ulaya katika mkesha wa Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO mjini Brussels. Kwenye ukurasa wa Twitter rais Trump amekosoa washirika wa Ulaya kuweka vikwazo vya kibiashara dhidi ya Marekani, na kutochangia fedha za kutosha kwenye matumizi ya ulinzi ya NATO. Rais Trump aliwasili Brussels jana jioni kuhudhuria mkutano wa kilele wa NATO utakaofanyika leo na kesho, na baadaye anatarajiwa kufanya ziara nchini Uingereza na halafu kukutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin mjini Helsinki, Finland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako