• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuimarisha ushirikiano na Afrika katika ulinzi na usalama

  (GMT+08:00) 2018-07-11 09:55:13

  Waziri wa ulinzi wa China Jenerali Wei Fenghe amekutana na wajumbe 49 kutoka nchi za Afrika kwenye mkutano wa kwanza wa baraza la ulinzi na usalama kati ya China na Afrika mjini Beijing, ambako amesisitiza ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye mambo ya ulinzi na usalama.

  Bw. Wei amesema matokeo yanayotokana na ushirikiano huo yatasaidia kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika.

  Mkutano wa Baraza hilo ulioanzia tarehe 26 Juni na kufungwa jana, ulihudhuriwa na wajumbe kutoka China, nchi za Afrika na Umoja wa Afrika. Kwenye mkutano huo wamefikia makubaliano kuhusu mausala ya jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja, na uhusiano wa kijeshi katika zama mpya. Wajumbe wa Afrika wameeleza matumaini yao ya kukuza ushirikiano wa kiutendaji kati ya pande mbili kwenye nyanja zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako