• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wasema utafuatilia kwa karibu uchaguzi wa Zimbabwe

  (GMT+08:00) 2018-07-11 09:55:37

  Umoja wa Afrika umesema utafuatilia kwa karibu uchaguzi wa rais, wabunge na serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 30 mwezi huu nchini Zimbabwe.

  Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema kutokana na mwaliko wa serikali na tume ya uchaguzi ya Zimbabwe, ujumbe wa waangalizi wa umoja huo umetumwa nchini humo.

  Taarifa imeongeza kwamba uchaguzi wa kuaminika, wa kidemokrasia na wa amani, ni muhimu ili kuendana na matumaini ya Umoja wa Afrika na kutimiza mafungamano ya nchi za Afrika, na amani na ustawi barani Afrika.

  Ujumbe huo wa waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika uliwasili Zimbabwe wiki iliyopita, na utafuatilia mchakato mzima wa uchaguzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako