• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Dunia: Ufaransa yafuzu fainali kwa kuifunga ubeligiji

  (GMT+08:00) 2018-07-11 10:15:38

  Matumaini ya timu ya taifa ya Ubelgiji ya kufika fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia yameshindikana baada ya kufungwa na Ufaransa jana kwenye mechi ya Nusu Fainali.

  Ufaransa ilishinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Sammy Umtiti kunako dakika ya 51 ambaye aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga goli la Ushindi kwenye mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia, kwani ana miaka 24 na miezi 7, akivunja rekodi iliyowekwa miaka 60 iliyopita na mchezaji Just Fountaine wa Ufaransa aliyefunga mwaka 1958 akiwa na miaka 24 na miezi 10.

  Kutokana na ushindi huo Ufaransa sasa inafuzu Fainali ya Kombe la Dunia na sasa itakutana na mshindi wa mechi ya pili ya Nusu Fainali ya pili kati ya Croatia na Uingereza itakayopigwa leo mjini Moscow.

  Lakini Ubeligiji nao watacheza mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya timu itakayofungwa kwenye mechi hiyo ya leo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako