• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kuhimiza uzalishaji viwandani ili kuongeza uuzaji bidhaa nje

  (GMT+08:00) 2018-07-11 10:16:06

  Katibu mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda ya Kenya Bw Chris Kiptoo amesema Kenya inapanga kuhimiza sekta ya uzalishaji viwandani ili kuongeza uuzaji bidhaa nje, kwani chapa nyingi za kimataifa ni katika bidhaa zilizotengenezwa na wala sio malighafi.

  Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya Wiki ya Biashara ya Kenya kufanyika kuanzia Julai, 29 hadi Agosti mosi, Bw. Kiptoo amesema ili kuhimiza uuzaji bidhaa nje, Kenya inatakiwa kuimarisha sekta ya uzalishaji viwandani kwa kuongeza mchango wake kwa Pato la Ndani GDP kutoka asilimia 10 hadi asilimia 20, ambao haukuwa mzuri katika miaka kadhaa iliyopita, kutokana na changamoto mbalimbali kama vile gharama kubwa za uzalishaji.

  Ameongeza kuwa serikali inatekeleza mageuzi mbalimbali ikiwemo kupunguza gharama za umeme ili kufanya Kenya iwe kituo cha uzalishaji viwandani chenye nguvu kwenye ushindani wa kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako