• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Raia 232 wauawa katika mashambulizi Sudan Kusini katika miezi miwili iliyopita

  (GMT+08:00) 2018-07-11 10:16:29

  Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limesema raia 232 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa katika maeneo ya Mayendit na Leer na watu binafsi kutoka serikali ya Sudan Kusini, vikosi vinavyoiunga mkono serikali na vijana wenye silaha wanaotoka maeneo yanayodhibitiwa na wapinzani kuanzia Aprili, 16 hadi Mei, 24.

  Baraza hilo limesema katika ripoti yake kuwa uchunguzi umetambua watu watatu wanaotuhumiwa kuwa watekelezaji wakuu wa mauaji hayo, mmoja wao ameripotiwa kuondolewa kwenye nafasi yake kwa tuhuma za kujihusisha na matukio hayo.

  Kamishna mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Bw. Zeid Ra'ad Al Hussein ameitaka serikali isimamishe mashambulizi yote dhidi ya raia, kuanzisha uchunguzi na kuwachukulia hatua wahalifu wakiwemo wale wanaowajibika kutoa amri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako