• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yalaani Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa zaidi za China 

  (GMT+08:00) 2018-07-11 17:10:05
  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China bibi Hua Chunying amesema hatua ya Ofisi ya wajumbe wa biashara ya Marekani kutoa orodha ya bidhaa nyingine za China zenye thamani ya dola bilioni 200 za kimarekani zitakazoongezewa ushuru wa forodha, inalenga kukandamiza China kibiashara..

  Bibi Hua amesema China itachukua hatua ya kulinda maslahi yake halali, na kwamba vita ya kibiashara iliyoanzishwa na Marekani ni vita kati ya upande mmoja na pande nyingi, ni vita kati ya kitendo cha kujilinda kibiashara na biashara huria, na pia ni vita kati ya umwamba na utaratibu. Amesema China itashirikiana na jumuiya ya kimataifa kulinda utaratibu wa biashara wa pande nyingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako