• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zambia kuongeza hifadhi za taifa ili kustawisha sekta ya utalii

  (GMT+08:00) 2018-07-11 19:17:32

  Serikali ya Zambia jana imesema itaongeza wanyama katika hifadhi tano za taifa mwaka huu ili kuimarisha sekta ya utalii nchini humo.

  Katibu mkuu wa wizara ya utalii na utamaduni ya Zambia Howard Sikwela amesema, aina 1,361 za wanyamapori wataongezwa kwenye hifadhi za taifa, wakiwemo Viboko weupe, Viboko weusi, Swala, Nyati, Pundamilia na Kongoni. Amesema, kuongeza idadi ya wanyamapori kutakuwa na gharama kubwa, lakini serikali ya Zambia inapaswa kufanya hivyo ili kustawisha sekta ya utalii nchini humo.

  Ameongeza kuwa, baadhi ya aina za wanyamapori katika bustani za taifa wametoweka kutokana na shughuli za binadamu kama vile uwindaji haramu, na hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wanyamapori.

  Z

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako