• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Korea Kaskazini yapata maendeleo katika nyanja ya haki za binadamu

  (GMT+08:00) 2018-07-11 19:18:48

  Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya binadamu Mark Lowcock amesema, Korea Kaskazini imepata mafanikio katika mchakato wa haki za binadamu tangu mwaka 2012, ingawa bado kuna changamoto za utapiamlo kwa watoto na ukosefu wa maji safi na vifaa vya tiba.

  Bw. Lowcock amesema hayo katika ziara ya kwanza ya msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Korea Kaskazini katika miaka saba. Akiwa nchini Korea Kaskazini, Bw. Lowcock ametembelea hospitali, shule ya chekechea na mashamba katika mkoa wa Hwanghae Kusini nchini humo.

  Amesema Korea Kaskazini itapewa msaada wa dola za kimarekani milioni 110 kupitia misaada kutoka kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako