• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msako wa mashine za kamari waendelea Kenya

  (GMT+08:00) 2018-07-11 20:43:55
  Serikali nchini Kenya inaendeleza vita dhidi ya kamari za haramu kwa nia ya kuwaepusha wanafunzi na michezo hiyo iliyowavutia sana baada ya maeneo mengi ya Kamari kuanzishwa kote nchini.

  Kwa miezi kadhaa sasa serikali imeendeleza msako wa mashine za kamari ambazo hazina leseni.

  Msako huo sasa umelekezwa katika kaunti ya Kwale,Pwani ya Kenya,ambapo kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo maafisa wa polisi eneo la Lungalunga jana walifanikiwa kuwatia mbaroni wacheza kamari za karata watatu katika soko la Mwangulu ambapo wanawahadaa na kuwapora pesa wafanyabiashara na wanafunzi.

  Ngumo alisema amesema mchezo huo wa kamari sio halali na hataruhusu kuchezwa katika sehemu yeyote ya kaunti hio akisema kuwa oparesheni ya kuzisaka machine za kamari bado inaendelezwa na atakayepatikana atachukuliwa hatua za kisheria.

  Aidha amedokeza kuwa watatu hao wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kwale ili kufunguliwa mashtaka ya kuendeleza biashara haramu ya kamari .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako