Ubunifu huo wa usindikiaji mvinyo kutoka kwa karoti umemfanya kijana huyo wa miaka 30,kwa jina Mark Niigeza kutoka chuo kikuu cha Adventisti Kigali Rwanda kuwa maarufu.
Wengi wa wafanyabiashara wameahidi kumsaidia kupata soko la bidhaa yake hiyo.
Uzalishaji wa mvinyo huo ulianza Februari mwaka huu.
Niigeza amesema kwamba anatumia mashine maalum kutoka China pamoja na vifaa vingine vinavyomsaidia katika uzalishaji wa mvinyo huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |