• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya TADB yatoa mikopo ya Sh.bilioni 120 kwa wakulima

  (GMT+08:00) 2018-07-11 20:44:29
  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ,imesema mwaka huu inatarajia kutoa mikopo ya Sh.bilioni 120 kwa wakulima nchini Tanzania.

  Hadi mwisho wa mwaka jana,Benki hiyo ilitoa mikopo ya Sh.bilioni 11 kwa wakulima mbalimbali nchini humo.

  Mkurugenzi wa Fedha na Tehama wa TADB,Severin Ndaskoi,akizungumza na waandishi wa habari jana katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam ,alisema wameongeza kiwango cha mikopo kwa sababu wamemaliza kazi ya kujenga miundombinu.

  Alisema hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu,walishatoa mikopo ya Sh.bilioni 45 na ifikapo Desemba mwaka huu watakuwa wamefikia Sh.bilioni 120.

  Aidha alisema Benki hiyo inaendelea kushirikiana na benki za biashara ili kufikisha mikopo kirahisi kwa wakulima nchini Tanzania.

  Alisema lengo ni kuwainua wakulima kupitia benki za biashara ambazo zinawafikia kirahisi watu wengi nchini humo na wakulima wapate huduma hiyo mapema.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako