• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Algeria yawafukuza wahamiaji 355 haramu kutoka Niger

  (GMT+08:00) 2018-07-12 08:48:00

  Baraza la haki za binadamu la Algeria limesema Algeria imewafukuza wahamiaji haramu 355 kutoka Niger, na kuwarudisha nyumbani. Taarifa iliyotolewa na baraza hilo inasema, operesheni hiyo imefuatiliwa na vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa, na kusimamiwa na waangalizi kutoka mashirika ya Umoja wa mataifa nchini humo, ikiwemo shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR na Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Taarifa hiyo pia imetoa wito kwa watendaji wote wa suala la uhamiaji kutafakari kwa kina kuhusu ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la uhamiaji haramu, unaozikabili nchi kadhaa, ikiwemo Algeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako