• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa Uingereza aahidi kuwa Uingereza itaendelea kuwa mshirika mkubwa wa Marekani

  (GMT+08:00) 2018-07-12 08:48:20

  Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema Uingereza itaendelea kuwa mshirika thabiti na mkubwa wa Marekani, wakati alipojiandaa kukaribisha ziara ya rais Donald Trump wa Marekani atakayewasili Uingereza leo alasiri. Taarifa iliyotolewa jana usiku na ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza inasema Bibi May atatumia fursa ya ziara ya rais Trump, ambayo ni ya kwanza kwake nchini Uingereza, kusisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na ushirikiano wa karibu kati yao kwenye nyanja za ulinzi, usalama na sera za mambo ya nje, na kwamba Bibi May atajadiliana na rais Trump kuhusu kuimarisha uhusiano wa nchi mbili kwenye sekta za biashara na uwekezaji katika siku zijazo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako