• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Asilimia 94 ya watanzania wanatumia simu za mkononi

  (GMT+08:00) 2018-07-12 08:48:40

  Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Bw. Atashasta Nditiye amesema asilimia 94 ya watanzania wanatumia huduma za simu ya mkononi, na wizara yake itafanya juhudi kuhakikisha asilimia 6 inayobaki wanapata huduma hizo ndani ya muda mfupi. Kwa mujibu wa ofisa huyo, zaidi ya asilimia 70 ya watu wa Tanzania bado hawajatumia huduma za mtandao wa Internet. Bw. Nditiye amesema wizara yake inafanya kazi kuboresha huduma za Internet kwenye shule za umma, ambazo ametaja kuwa zitasaidia kutatua changamoto za upungufu wa walimu kwa kuwa zitawawezesha wanafunzi wajifunze kupitia mtandao wa Internet.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako