• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Michuano ya Kombe la Dunia 2018: Croatia yaungana na Ufaransa Fainali, yaichapa Uingereza 2-1

  (GMT+08:00) 2018-07-12 09:49:33

  Timu ya taifa ya England imeaga michuano ya Kombe la Dunia kwa kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Croatia kwa idadi ya mabao 2-1.

  Katika mchezo huo, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 na kuamuriwa kuongezwa dakika30 za ziada ili kupata mshindi.

  England walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 5 ya mchezo kwa njia ya mpira wa adhabu uliopigwa na kuwekwa kimiani na Kieran Trippier na baadaye kipindi cha pili Croatia walisawazisha kupitia kwa Ivan Perisic dakika ya 68.

  Croatia walizitumia vyema dakika za nyongeza kwa straika wake, Mario Mandzukic kuandika bao la pili kwenye dakika ya 106.

  England sasa itakutana na Ubelgiji kusaka mshindi wa tatu Jumamosi huku Croatia ikiungana na Ufaransa kucheza fainali Jumapili ya wiki hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako