• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kombe la Kagame: Wekundu wa Msimbazi watinga fainali, kukutana na Azam FC

  (GMT+08:00) 2018-07-12 09:50:29

  Goli pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere limetosha kuipa Simba Sports Club ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar jana jioni uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

  Kwa ushindi huo Simba inakwenda fainali ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu Kombe la Kagame na itakutana na Azam FC katika fainali itakayopigwa Kesho Ijumaa uwanja wa Taifa.

  Azam nayo imetinga fainali hizo kwa kuichapa Gor Mahia ya Kenya magoli 2-0. Mchezo wa fainali utakuwa wa kuvutia kutokana na historia ya timu hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako