• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yapitia sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuhimiza usimamizi

  (GMT+08:00) 2018-07-12 10:08:58

  Serikali ya Tanzania inapitia sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2001 ili iendane na mabadiliko kwa lengo la kuhimiza usimamizi wa uendeshaji wa mashirika hayo.

  Katibu mkuu wa kamati ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya taifa Bw. Ismael Suleiman, amesema marekebisho ya sheria hiyo yatatoa adhabu kali kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yenye mienendo mibaya, ikiwa ni pamoja ya kutafutia usajili.

  Habari kuhusu kupitia sheria hiyo imetolewa siku chache baada ya rais John Magufuli kumwamuru waziri wa mambo ya ndani Bw. Kangi Lugola kuangalia baadhi ya mashirika aliyotaja kuendeshwa kinyume cha sheria.

  Kwa mujibu wa takwimu za serikali, hivi sasa Tanzania ina mashirika laki 1.7 yasiyo ya kiserikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako