• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza kujenga dhana mpya ya usalama ili kutatua changamoto zinazohusiana na hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-07-12 10:09:27

    Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amehimiza jumuiya ya kimataifa kujenga dhana mpya ya usalama, ili kukabiliana na changamoto zinazohusiana na hali ya hewa.

    Amesema hayo wakati akishiriki kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya baraza la usalama la Umoja huo. Pia amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kujenga dhana mpya ya pamoja ya usalama endelevu ili kutatua kwa hatua mwafaka changamoto zinazotokana na hali ya hewa.

    Aidha, naibu katibu mkuu wa umoja huo Bibi Amina Mohammed amesisitiza uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa, na amani na usalama wa kimataifa, huku akitoa wito kuchukua hatua za pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako