• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yawarudisha raia 3,000 waliokwama nchi za nje

    (GMT+08:00) 2018-07-12 10:11:59

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw. Meles Alem amesema, Ethiopia imewarudisha raia 3,000 waliokwama katika nchi za nje katika miezi mitatu iliyopita.

    Bw. Alem amesema raia hao walirudishwa kutoka Falme za kiarabu, Kenya, Djibouti na Sudan. Amesema tangu waziri mkuu mpya wa nchi hiyo Bw. Abiy Ahmed alipoingia madarakani mwezi Aprili, nchi hiyo imepata mafanikio katika kuwarudisha wananchi wasio na hati, ambao wanaishi katika nchi za nje.

    Msemaji huyo pia amesema juhudi za Bw. Ahmed za kuwawezesha wananchi wake wanaoishi katika nchi za nje kurejea nyumbani, imekuwa sehemu ya mchakato wa mageuzi nchini Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako