• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Syria yajibu mashambulizi mapya ya Israel huko Guneitra

  (GMT+08:00) 2018-07-12 10:12:32

  Shirika la habari la serikali ya Syria SANA limesema, Jeshi la anga la Syria limejibu mashambulizi mapya yaliyofanywa na Israel dhidi ya Quneitra, mkoa wa kusini nchini Syria.

  Ndege za kivita za Israel zilirusha maroketi kadhaa katika vituo vya kijeshi vya Syria karibu na miji ya Hadar na Tal Kurum Jaba, kitongoji cha Quneitra, na kusababisha uharibifu, na jeshi la anga la Syria lilichukua hatua za kujibu mashambulizi hayo.

  Mashambulizi hayo ya Israel yamekuja wakati jeshi la Syria liliposhambulia eneo linalodhibitiwa na kundi la Khalid Bin al-Walid ambalo linahusiana na kundi la IS, kusini mwa Syria karibu na eneo la juu la Golan linalodhibitiwa na Israel. Upande wa Syria siku zote unailaani Israel kuunga mkono makundi yenye siasa kali katika sehemu ya kusini mwa Syria.

  Habari nyingine zinasema waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amesema kwenye mazungumzo kati yake na rais Vladimir Putin wa Russia huko Moscow, kuwa Israel itamchukulia hatua thabiti mtu yeyote anayejaribu kuingilia mipaka yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako