• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya CPC na vyama vya siasa vya Afrika kufanyika Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-07-12 10:24:49

  Mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na vyama vya siasa duniani kanda ya Afrika yatafanyika tarehe 17 na 18 mwezi huu mjini Dar es Salaam, Tanzania.

  Kauli mbiu ya mkutano huo ni "nadharia na uzoefu wa vyama vya siasa vya China na vya nchi za Afrika katika kutafuta njia za kujiendeleza zinazoendana na hali halisi ya nchi", na viongozi wa vyama na makundi 40 ya siasa ya Afrika watahudhuria mazungumzo hayo.

  Mazungumzo hayo ni shughuli muhimu ya kutekeleza pendekezo la kuanzisha utaratibu wa mazungumzo hayo lililotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye mazungumzo kati ya CPC na vyama vya siasa duniani yaliyofanyika mwezi Desemba mwaka jana, na pia yanalenga kutoa uratibu kwa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mjini Beijing.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako