• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashirika mengi zaidi ya Marekani yaja China kutafuta ushirikiano licha ya vita ya kibiashara kupamba moto

  (GMT+08:00) 2018-07-12 11:41:31

  Imetimia wiki tangu vita ya kibiashara kati ya China na Marekani ilipoanza, na mabadiliko mapya yameendelea kuibuka.

  Tarehe 10 usiku, Ofisi ya mwakilishi wa biashara wa Marekani ilitangaza orodha ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 za kimarekani zitakazotozwa ushuru wa asilimia 10, kwa kisingizio kuwa "China imechukua hatua za kulipiza kisasi na haijabadilisha mienendo yake kwenye biashara". Kuhusu orodha hiyo, wizara ya biashara ya China imesema hatua hiyo ya Marekani haikubaliki, na serikali ya China italazimika kuijibu kwa hatua madhubuti, ili kulinda maslahi ya nchi na watu wake.

  Kuanzia dola bilioni 50 hadi bilioni 200, kama orodha hizo zote zitatekelezwa, inamaanisha kuwa nusu ya biashara kati ya China na Marekani zitafungwa.

  Wakati huohuo licha ya kupamba moto kwa vita hiyo ya kibiashara, makampuni mengi zaidi ya Marekani yamekuja China kutafuta ushirikiano. Tarehe 10, kampuni ya magari ya umeme ya Tesla ya Marekani imesaini makubaliano ya kujenga kiwanda chake cha kwanza nje ya Marekani mjini Shanghai, ambacho kinatarajiwa kuweza kuzalisha magari laki tano kwa mwaka. Tarehe 11, ujumbe wa wafanyabiashara wa Marekani unaoongozwa na meya wa Chicago Rahm Emanuel ulisaini makubaliano na China kuhusu ushirikiano wa miaka mitano ijayo katika sekta za afya, uvumbuzi, huduma za fedha, kilimo na chakula na miundombinu.

  Kwa upande mmoja Marekani inaendelea kutoza ushuru dhidi ya bidhaa za China, kwa upande mwingine makampuni makubwa ya Marekani yanaendelea kutafuta ushirikiano na China, hali ambayo inaakisi kuwa ingawa serikali kuu ya Marekani inazidi kukumbatia sera za kujilinda kibiashara, makampuni na serikali za majimbo wanapinga kivitendo vita ya kibiashara, na kuonesha imani na soko la China.

  Hali hiyo pia inaonesha kuwa wanasiasa na wafanyabiashara wa Marekani wameanza kutambua wazi kwamba hatua za serikali ya Marekani kuzusha vita ya kibiashara ni kwa ajili ya maslahi ya chama, bila kujali maslahi ya umma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako