• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inaweza kushinda changamoto inayotokana na vita ya kibiashara iliyoanzishwa na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-07-12 19:02:07

    China inaweza kushinda changamoto inayotokana na vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani, kwa kupitia kutimiza maendeleo mazuri ya uchumi, kuboresha maisha ya watu na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

    Hivi sasa vita ya biashara kati ya China na Marekani inapamba moto, watu wana wasiwasi kuwa uchumi wa China na hata uchumi wa dunia unaweza kuathiriwa. Lakini China inaamini kuwa athari hiyo ni ndogo na ya muda mfupi, kwani ina uwezo wa kutosha wa kushinda changamoto zitakazotokana na vita hiyo. Kwanza, China ni nchi pekee yenye sekta zote za uzalishaji duniani, na pia ina soko kubwa la watu bilioni 1.4; pili, mahitaji ya ndani yamegeuka kuwa injini kubwa zaidi ya ongezeko la uchumi; tatu, maendeleo ya uvumbuzi ni mkakati mkuu wa China; na nne, China kufungua mlango zaidi kutanufaisha nchi marafiki za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako