• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Bidhaa za Kenya huchukua muda mrefu kufika Marekani

  (GMT+08:00) 2018-07-12 19:08:41
  Mauzo ya bidhaa za Kenya katika soko la Marekani yanaathiriwa na muda mrefu wa kusafirisha bidhaa hadi Marekani.

  Mkuu wa baraza ya kuuza bidhaa nje nchini Kenya Jas Bedi, amesema mjini Washington kwamba inachukua siku 135 kufikisha bidhaa za Kenya nchini Marekani na hivyo kuchelewesha wateja.

  Alisema kwa biashara ya kisasa huo ni muda mrefu sana ikilinganishwa na siku 45 ambazo China kufikisha bidhaa kwa soko la Marekani.

  Kulingana na Bedi, muda mwingi unapotea kutokana na safu ndefu ya kuagiza maligafi na kutengeneza bidhaa kabla ya kuzisafirisha.

  Mauzo ya bidhaa za Kenya kupitia kwa AGOA nchini Marekani yalifikia dola milioni 349 mwaka 2015 lakini hadi mwaka jana yalipungua na kufikia dola milioni 325.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako