• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Maonyesho ya 42 ya  Sabasaba  yaongezwa muda

  (GMT+08:00) 2018-07-12 19:27:38
  Maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara ya (Sabasaba) nchini Tanzania yaliyotarajiwa kumalizika Julai 13, yameongezwa siku mbili hivyo yatamalizika Julai 15.

  Kuongezeka kwa siku hizo mbili kunafanya maonyesho hayo yaliyoanza Juni 28, mwaka huu kudumu kwa siku 18.

  Akizungumza na waandishi wa habari, katika maonyesho hayo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(Tantrade), Edwin Rutageruka ametaja sababu ya kuongeza siku za maonesho hayo kuwa ni kutokana na maombi ya wadau.

  Aidha amesema sababu nyingine ni kuwapa nafasi zaidi wale ambao hawakupata fursa ya kutembelea maonesho hayo kufanya hivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako