• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbizi wa Syria wanaorejea makwao kutoka Lebanon waongezeka kwa asilimia 30 katika miezi miwili

    (GMT+08:00) 2018-07-12 19:30:24

    Idadi ya Wasyria wanaorejea makwao kutoka Lebanon imeongezeka kwa asilimia 30 katika miezi miwili iliyopita ikilinganishwa na mwaka jana.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Syria Muhammad al-Sha'ar amesema, kuongezeka kwa kiwango cha wakimbizi wanaorejea kunatokana na utulivu na amani ambayo imepatikana hivi karibuni, na pia ahueni wanayohisi watu wa Syria kutokana na ushindi wa jeshi la serikali ya nchi hiyo.

    Mapema mwezi huu, wizara ya mambo ya nje ya Syria iliwataka Wasyria waliokimbia nchi hiyo kurejea makwao, na kuyataka mashirika ya kimataifa kubeba wajibu wao katika kuratibu watu hao kurejea nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako