• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yatoa taarifa kuhusu Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2018-07-13 07:18:24

    Wizara ya biashara ya China imetoa taarifa kuhusu Tangazo la uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani lililotolewa tarehe 10 na Ofisi ya wawakilishi wa biashara ya Marekani.

    Taarifa hiyo imesema kauli ya Marekani kuhusu China kupata faida zaidi katika ushirikiano wa uchumi na biashara kwa njia isiyo ya haki imepotosha ukweli wa mambo na haina msingi wowote. Imesema matatizo yaliyopo kwenye jamii na uchumi nchini Marekani yamesababishwa na masuala ya kimuundo, na mafanikio ya uchumi wa China yamepatikana kwa kutegemea sera madhubuti za kusukuma mbele mageuzi na kufungua mlango.

    Taarifa pia imesema China siku zote inazingatia mikwaruzano kati ya pande hizo mbili katika sekta ya uchumi na biashara, na kufanya juhudi kubwa katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo. Imesema kitendo cha Marekani cha kuzusha vita vya kibiashara kimehatarisha uchumi wa dunia, kuleta msukosuko wa soko, na kuharibu maslahi ya kampuni nyingi na wateja wa kawaida.

    Pia imesisitiza kuwa China itashikilia kithabiti mageuzi na ufunguaji mlango, na itaendelea kushirikiana na nchi mbalimbali katika kulinda kanuni ya biashara huria na mfumo wa biashara ya pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako