• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiongozi wa UN aahidi kuendelea na juhudi za kutokomeza udhalilishaji wa kijinsia

  (GMT+08:00) 2018-07-13 08:58:31

  Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ameahidi kuendelea na juhudi za kutokomeza udhalilishaji wa kijinsia kwenye mfumo wa umoja huo. Akikutana na wanahabari kwenye makao makuu ya Umoja huo, Bw. Guterres amesisitiza msimamo wa kutovumilia hata kidogo udhalilishaji wa kijinsia, na pia ametaja hatua kadhaa zitakazochukuliwa dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia kwenye sekritarieti ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na kuunda timu maalumu ya wachunguzi, kutekeleza utaratibu wenye ufanisi wa kupokea, kushughukilia na kutatua malalamiko, kuweka namba maalumu ya simu kwa ajili ya kuripoti udhalilishaji wa kijinsia, na kurekebisha mafunzo ya lazima juu ya udhalilishaji wa kijinsia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako