Umoja wa Ulaya unapanga kuimarisha ulinzi wa mpaka wake kwa kuunda kikosi chenye walinzi wa mpaka elfu kumi ifikapo mwaka 2020 na kikosi cha polisi wa mpakani. Kamishna wa uhamiaji wa Umoja wa Ulaya Bw. Dimitris Avramopoulos amesema hayo baada ya kukutana na mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi wanachama wa Umoja huo nchini Austria mapema jana. Mawaziri hao wamekutana kujadili msukusuko wa wahamiaji, ambao umekuwa tatizo kubwa kwa Umoja wa Ulaya tangu ulipoanza mwaka 2015.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |