• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanamazingira wa Kenya watembea kwa miguu kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya uhifadhi wa tembo na faru

  (GMT+08:00) 2018-07-13 08:59:37

  Kundi la wanamazingira kumi wa Kenya wanapanga kutembea kwa miguu kwenda Afrika Kusini, kwa lengo la kuinua mwamko wa umma kuhusu uhifadhi wa tembo na faru. Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Elephant Neighbor Center Bw. Jim Nyamu amesema mjini Nairobi kuwa anapanga kutembea kwa miguu kutoka Kenya kwenda Afrika Kusini kupitia Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe na Botswana kwa kipindi cha siku 160. Amesema kutembea huko kumekuja wakati ushoroba wa tembo unashuhudia kupungua kwa kasi kwa idadi ya tembo kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za wanyamapori kote duniani, na unalenga kuunga mkono marufuku dhidi ya biashara ya pembe za ndovu na kuomba kuweka sheria kali za kupambana na ujangili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako