• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan arefusha muda wa kusimamisha mapambano kwenye maeneo yote yenye mgogoro

    (GMT+08:00) 2018-07-13 09:13:47

    Rais Omar Al Bashir wa Sudan ametangaza amri ya kurefusha muda a kusimamisha mapambano kwenye maeneo yote yenye migogoro nchini Sudan hadi mwishoni mwa mwaka huu.

    Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Sudan inasema uamuzi huo umefikiwa kutokana na msimamo wa serikali kufuata amani na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye majadiliano ya kitaifa. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa serikali ya Sudan Kusini na wapinzani wenye silaha wamekuwa wakirefusha makubaliano ya kusimamisha vita kwenye maeneo yenye migogoro.

    Mwaka 2016 Rais Omar Al Bashir alitangaza kusimamisha vita kwa miezi minne ili kuwawezesha waasi wajiunge na majadiliano kuhusu amani ya taifa, makubaliano hayo yamekuwa yakirefushwa mara kwa mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako