• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Guterres asema ataahirisha ziara yake kama Rais Kabila atatangaza maamuzi sahihi

  (GMT+08:00) 2018-07-13 09:14:14

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema yuko tayari kuahirisha ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kama hatua hiyo ina maana kuwa Rais Kabila atatangaza jambo zuri.

  Bw. Guterres na Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Mousa Mahmat walipanga kufanya ziara wiki hii mjini Kinshasa kukutana na Rais Joseph Kabila. Lakini ziara hiyo imeahirishwa kwa kuwa Rais Kabila anatarajia kutangaza maamuzi muhimu hivi karibuni na hataki ionekane kama anafanya hivyo kutokana na shinikizo la kimataifa.

  Rais Kabila alimaliza muda wa kuwa madarakani mwezi Desemba mwaka 2016, na amekuwa akipata shinikizo la kimataifa kuondoka madarakani. Kwa sasa uchaguzi wa Rais na bunge nchini humo umepangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako