Croatia imeendelea kusheherekea ushindi wake dhidi ya Uingereza Jumatano wiki hii, baada ya timu hiyo kuwaadhabu Uingereza baada ya muda wa ziada kwa magoli 2-1.
Mashabiki wa Croatia walisherehekea usiku kucha baada ya taifa lao kuwaondoa England kutoka kwa michuano ya Kombe la Dunia Urusi na kufuzu kwa fainali kwa mara yao ya kwanza kabisa. WAkati huo huo Uingereza imeendelea kuomboleza kipigo cha mabao mawili kwa bao lao la kufutia machozi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |