• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu Tanzania Bara (VPL): TFF yaruhusu wachezaji wa kigeni kufikia 10

    (GMT+08:00) 2018-07-13 09:47:22

    Kamati ya utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imepitisha kanuni za kuruhusu usajili wa idadi ya wachezaji 10 wa kigeni katika ligi kuu kuanzia msimu ujao.

    Wachezaji hao wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja, katika ligi kuu na mashindano ya kimataifa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka ambapo timu zilikuwa zinaruhusiwa kutumia wachezaji saba pekee wa kigeni.

    Wakati huohuo, ikiwa imesalia mwezi mmoja pekee kuelekea msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara, bodi ya ligi hiyo kupitia mkurungezi wake Boniface Wambura, imesema tayari imeshakamilisha kupanga ratiba.

    Wambura amesema ratiba imezingatia mambo mengi ikiwemo mashindano ya CAF, FIFA ambayo mwaka huu yatakuwa yanaanza mwishoni mwezi disemba hivyo wameipanga kulingana na uwepo wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako