• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Morocco kuzindua treni ya mwendo kasi ya kwanza barani Afrika mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-07-13 09:47:54

  Kampuni ya reli ya Morocco ONCF imetangaza kuwa itazindua treni ya mwendo kasi ya kwanza barani Afrika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

  Kampuni hiyo imetoa taarifa ikisema, jaribio la kiufundi la mradi huo wa reli ya mwendo kasi ambao unaunganisha miji ya Tangier na Casablanca ulikamilika mwezi wa Juni.

  Kwa mujibu wa kampuni hiyo, treni hiyo ambayo ni ya kisasa na yenye maendeleo na ubunifu, itakuwa ni taswira ya nchi inayoelekea kujenga mustakbali mzuri.

  Treni hiyo mpya yenye mwendo kasi zaidi ya kilomita 352 kwa saa katika majaribio, itapunguza muda wa safari kati ya Tangier na Casablanca kutoka saa 5 hadi 2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako