• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UM asisitiza utaratibu wa pande nyingi na mahusiano ya kimataifa yaliyojengwa kwenye msingi wa kanuni

  (GMT+08:00) 2018-07-13 09:48:24

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza umuhimu wa utaratibu wa pande nyingi na mahusiano ya kimataifa yaliyojengwa kwenye msingi wa kanuni, katika kukabiliana na changamoto za kimataifa.

  Bw. Guterres amesema hayo wakati akizungumzia wasiwasi wake kuhusu Marekani kukiuka utaratibu wa kimataifa uliowekwa baada ya vita vya dunia vya pili, Umoja wa Mataifa ukiwa ni sehemu ya msingi wake.

  Pia amesema, anaamini kuwa dunia itaendelea kutambua umoja huo kama chombo cha lazima cha pande nyingi kinachounga mkono amani na usalama wa dunia, na kuwa nguzo muhimu katika maendeleo na haki za binadamu.

  Ameongeza kuwa ana imani imara kuwa changamoto nyingi zinazoikabili dunia kwa sasa ni za kimataifa, na mfumo wa kimataifa unaofuata kauni na utaratibu wa pande nyingi, ni njia pekee ya kukabiliana na changamoto hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako