• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 12 wajeruhiwa katika mlipuko wa tanki la mafuta karibu na uwanja wa ndege wa Cairo, Misri

  (GMT+08:00) 2018-07-13 09:50:44

  Watu 12 wamejeruhiwa katika mlipuko wa tanki la mafuta karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cairo, nchini Misri lakini safari za ndege hazikuathirika.

  Duru za usalama zimeliambia shirika la habari la Misri MENA kuwa mlipuko huo ulitokea katika eneo la Heliopolis mjini Cairo.

  Waziri wa usafiri wa anga wa Misri Bw. Mohamed al-Masri amesema kwenye taarifa yake kuwa matanki mawili yalilipuka nje ya uwanja wa ndege. Pia amesema safari zote za ndege za ndani na za kimataifa zinaendelea kama kawaida, na chanzo cha mlipuko huo ni joto kali na moto umedhibitiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako