• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bunge la Sudan Kusini larefusha muhula wa rais kwa miaka mitatu

  (GMT+08:00) 2018-07-13 09:54:37

  Bunge la Sudan Kusini limeamua kurefusha muhula wa rais Salva Kiir na wa Serikali ya Mpito ya Umoja wa Kitaifa kwa miaka mingine mitatu hadi mwaka 2022, baada ya wabunge wa chama tawala cha SPLM kupiga kura za ndio kwa kauli moja.

  Waziri wa sheria wa Sudan Kusini Bw Paulino Wanawilla Unango mapema mwezi huu aliwasilisha mswada bungeni, akitafuta kurefusha kipindi cha serikali ya mpito, cha rais, cha makamu wa kwanza wa rais na magavana wa majimbo kwa miaka mingine mitatu, kinachotarajiwa kuisha mwezi Agosti kwa mujibu wa Makubaliano dhaifu ya Amani yaliyosainiwa mwaka 2015, kati ya rais Kiir na kiongozi wa waasi Bw. Riek Machar.

  Kundi kuu la waasi SPLM-IO linaloongozwa na Bw. Machar na makundi mengine ya upinzani hivi karibuni wameeleza kupinga kurefushwa kwa muda wa serikali ya mpito, wakisema inakwenda ni kinyume na moyo wa mazungumzo yanayoendelea kati ya makundi hasimu na juhudi za Shirika la Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD katika kuleta amani, ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa miaka zaidi ya minne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako