• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukweli kuhusu biashara kati ya China na Marekani hautapotoshwa na uongo

    (GMT+08:00) 2018-07-13 14:54:09

    Tarehe 10 ofisi ya mwakilishi wa biashara wa Marekani imetoa taarifa kuhusu uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani dhidi ya China, na kudai kuwa China imenufaika kwa njia zisizo haki kwenye biashara kati yake na Marekani. Lakini uongo ni uongo, na kuurudiarudia hakutaufanya uwe ukweli.

    Tarehe 12 wizara ya biashara ya China imetoa taarifa ikikanusha shutuma zisizo na msingi zilizotolewa na taarifa ya Marekani. Kwenye taarifa hiyo wizara ya biashara ya China imesema suala urari mbaya kwenye biashara linatokana na kiwango cha chini cha akiba nchini Marekani na hadhi ya dola ya kimarekani kuwa sarafu ya akiba ya kimataifa, na pia linatokana na Marekani kudhibiti uuzaji wa bidhaa za teknolojia ya hali ya juu kutokana na mawazo ya Vita baridi.

    Ikitaja shutuma ya kuiba hakimiliki iliyotolewa na Marekani dhidi ya China, wizara hiyo imesema hivi sasa China imekuwa na mfumo kamili wa sheria na kanuni za kulinda hakimiliki za ujuzi, na mahakama za hakimiliki zimeanzishwa katika miji ya Beijing, Shanghai na Guangzhou ambazo zinapokea mashtaka kutoka kwa makampuni ya nje. Shirika la hakimiliki duniani WIPO limetangaza hivi karibuni kuwa idadi ya maombi ya hataza yaliyowasilishwa na China imefikia elfu 51 na kuchukua nafasi ya pili duniani, baada ya Marekani, na inachotarajia China ni kwamba serikali za nchi za nje zitaimarisha ulinzi wa hakimiliki za China.

    Kuhusu tuhuma ya kulazimisha uhamishaji wa teknolojia, wizara hiyo imetaja kuwa madai hayo yenyewe ni "habari feki", na kusema kuwa nchini China hakuna sheria au kanuni yoyote zinazolazimisha uhamishaji wa teknolojia wakati mitaji ya nje inapoomba kuingia kwenye soka la China. Wizara hiyo imesisitiza kuwa uchumi wa soko ni uchumi unaojengwa kwenye msingi wa mikataba, na uhamishaji wa teknolojia pia ni biashara inayofanyika kwenye msingi wa makubaliano ya haki na usawa, kwa hivyo madai hayo ya Marekani hayana msingi kabisa.

    Inaonekana wazi kwamba hatua hizo ni jaribio la Marekani kukwamisha maendeleo ya China kwenye sekta za viwanda vya kisasa na teknolojia za hali ya juu, na pia zinaonesha wasiwasi wa Marekani juu ya maendeleo ya China, ambao unaifanya serikali yake ifanye juhudi zote kujaribu kumzuia mshindani wake kwenye ushindani wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako