• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 7-Julai 13)

  (GMT+08:00) 2018-07-13 17:07:15

  Vijana wote 12 na kocha wao waokolewa kutoka pangoni Thailand

  Vijana wote 12 na kocha wao wa mpira wa miguu wameokolewa kutoka kwenye pango lililofurika maji kaskazini mwa Thailand, baada ya kukwama ndani kwa siku 18.

  Kiongozi wa uratibu wa operesheni ya uokoaji Bw. Narongsak Osatanakorn, amesema wamekamilisha operesheni ya uokoaji, ambayo haikuwahi kufanikiwa duniani.

  Kundi la wataalamu zaidi ya mia moja wa kupiga mbizi walikuwa wakifanya kazi katika pango hilo, na wamekuwa wakiwaelekeza wavulana hao kwenye giza na maeneo yaliyofurika maji kwenda kwenye mlango wa pango hilo.

  Vijana hao 12 wa timu ya Wild Boar wenye umri wa kati ya miaka 11-16 waliingia katika mapango ya Tham Luang katika jimbo la Chiang Rai nchini Thailand wakiwa na mwalimu wao mwenye umri wa miaka 25

  Baada ya watoto hao kutoonekana nyumbani waliripotiwa kupotea na jitihada za kuwatafuta zikaanza.

  Wataalamu wa kupiga mbizi kutoka duniani kote waliwasili nchini humo kwa ajili ya kusaidia waokoaji.

  Hata hivyo hali ya simanzi ilijitokeza baada ya muokoaji mmoja aliyekuwa kwenye operesheni ya uokoaji alipofariki.

  Saman Gunan, mfanyakazi wa zamani wa kikosi cha majini alikuwa akijitolea pangoni, alipoteza fahamu walipokuwa anapeleka mitungi ya oksijeni


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako