• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 7-Julai 13)

  (GMT+08:00) 2018-07-13 17:07:15

  Watu takriban 80 wauawa katika mashambulizi kaskazini mwa Nigeria wiki hii

  Watu takriban 80 wamethibitishwa kuuawa katika mashambulizi tofauti yaliyotokea Jumatatu na Jumanne dhidi ya vijiji vya mpakani, kaskazini mwa Nigeria.

  Mbunge wa jimbo la Adamawa Bibi Sodomti Tayedi amesema watu zaidi ya 50 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia jamii kadhaa katika majimbo ya Adamawa na Taraba, kaskazini mashariki ya Nigeria. Amesema kutokana na wimbi la mashambulizi katika eneo la Numan, wakazi ambao wengi wao ni wakulima wamekimbia na kuacha mashamba yao.

  Wakizungumzia shambulizi jipya, wakazi wamesema watu wenye silaha waliwavamia walipokuwa katika soko la jioni la wikiendi.

  Wakati huohuo, Shirika la Kushughulikia Hali ya Dharura la Taifa limesema miili 26 ilipatikana kufuatia shambulizi la siku mbili linalodhaniwa kufanywa na washambuliaji katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako