• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 7-Julai 13)

  (GMT+08:00) 2018-07-13 17:07:15

  Serikali kupitia upya kodi ya mitandao ya kijamii Uganda

  Waziri mkuu wa Uganda amesema serikali itapitia upya kodi ya mitandao ya kijamii na miamala kwa njia ya simu

  Waziri Mkuu wa Uganda Bw. Ruhakana Rugunda amesema serikali ya Uganda itapitia upya kodi ya matumizi mitandao ya kijamii na miamala kwa njia ya simu, baada ya umma kutoa malalamiko kwa siku kadhaa.

  Bw. Rugunda ameliambia bunge kuwa wiki ijayo serikali itawasilisha marekebisho ya sheria ya ushuru ya mwaka 2018, inayotoza moja kwa moja kodi ya shilingi 200 za Uganda kila siku kwa matumizi ya mitandao ya kijamii, na ushuru wa asilimia 0.5 kwa miamala ya fedha kwa njia ya simu. Bw. Rugunda pia amesema Rais Yoweri Museveni amesikia kilio cha umma na kusema kodi hiyo itajadiliwa tena bungeni.

  Wiki hii polisi walitumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi za moto angani kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wanapinga kodi hiyo. Wanaharakati ikiwa ni pamoja na wabunge, wasanii, mabloga, wanahabari na jumuiya zisizo za kiserikali wanasema kodi hiyo si ya haki, ni kubwa na inazuia uhuru wa watu kutoa maoni.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako