• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 7-Julai 13)

  (GMT+08:00) 2018-07-13 17:07:15

  Ethiopia na Eritrea kuanzisha kamati za kitaifa ili kurejesha uhusiano

  Ethiopia na Eritrea zinapanga kuanzisha kamati za kitaifa kuhusu maeneo ya uchumi, siasa, usalama na jeshi.

  Akizungumza na vyombo vya habari mjini Addis Ababa muda mfupi baada ya kurudi kutoka Eritrea, waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Workneh Gebeyehu amesema mahusiano ya kiuchumi, kidiplomasia, kisiasa na binadamu ambayo yalisimamishwa kwa miaka 20, yatarejeshwa hivi karibuni.

  Ujumbe ulioongozwa na waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed nchini Eritrea, jana asubuhi ulisaini taarifa ya amani na Eritrea ili kumaliza uhasama, kushughulikia mgogoro wa mpaka na kuanzisha tena mahusiano ya kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

  Bw. Gebeyehu ameeleza kuwa kamati hizo za kitaifa zitaweka ratiba ya kutekeleza mpango huo na kwamba wameanzisha tume mbili zinazoongozwa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili.

  Wakati huo huo katibu mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD amepongeza mkutano wa kihistoria kati ya viongozi wa Ethiopia na Eritrea baada ya uhasama uliodumu kwa miaka 20.

  Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed jana alikuwa kiongozi wa kwanza kufanya ziara nchini Eritrea katika miaka zaidi ya 20 iliyopita.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako