• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 7-Julai 13)

  (GMT+08:00) 2018-07-13 17:07:15

  Chama tawala cha Rwanda chapitisha majina 70 kwa ajili ya uchaguzi ujao wa wabunge

  Chama tawala cha Rwanda RPF kimepitisha majina ya wagombea 70 watakaoshiriki kwenye uchaguzi ujao wa bunge, unaotarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.

  Orodha ya majina ya wagombea waliochaguliwa ilitangazwa kwenye mkutano wa kamati kuu ya chama uliohudhuriwa na wajumbe karibu 2,000 ikiwa ni pamoja na Rais Paul Kagame.

  Katibu Mkuu wa chama cha RPF Bw. Francois Ngarambe, alisoma orodha ya majira ya wagombea ikiwa na wale ambao bado ni wabunge na wengine wapya. Bw Ngarambe amesema chama chake kimeteua wagombea 80 kwa jumla, lakini kimeamua kuacha nafasi nyingine 10 kwa ajili ya vyama vingine.

  Tume ya uchaguzi ya Rwanda imesema uchaguzi wa baraza la chini wa bunge la Rwanda unatarajiwa kufanyika tarehe 2 hadi 4 Septemba.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako