• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sera ya "kutoa soko kwa kupata teknolojia" hakupaswi kupakwa matope

    (GMT+08:00) 2018-07-13 17:23:31

    Mikwaruzano ya biashara kati ya China na Marekani inapamba moto. Marekani imeilaumu China kwa visingizio vingi, na moja ya visingizio ni sera inayotekelezwa na China ya "kutoa soko kwa kupata teknolojia". Wachambuzi wanaona kuwa sera hiyo ni ya kunufaishana, haipaswi kupakwa matope.

    Mtaalamu wa idara ya utafiti wa uchumi wa nje ya kituo cha utafiti wa maendeleo ya baraza la serikali la China Bw. Zhang Qi amesema, nchi nyingi duniani zinatoa soko kwa nchi nyingine kwa sharti la kupata teknolojia, na hili ni chaguo la kunufaishana. Marekani inatilia maanani sana ushirikiano wa kimataifa wa sayansi na teknolojia. Mwaka 1999, kamati ya sayansi na teknolojia ya Marekani ilitoa ripoti ikisema, umuhimu wa ushirikiano huo unatokana na mahitaji muhimu ya Marekani katika kulinda usalama na kudumisha hadhi ya uongozi duniani. Licha ya Marekani, Japan na Korea ya Kusini pia ni mifano mizuri ya utekelezaji wa sera ya "kutoa soko kwa kupata teknolojia". Nchi hizo mbili ziligeuka kuwa nchi zilizoendelea kwa kujifunza teknolojia za hali ya juu ya nchi za zilizoendelea ikiwemo Marekani.

    Bw. Zhang amesema China imefuata vizuri kanuni za kimataifa katika "kutoa soko kwa kupata teknolojia". Kuanzia mwaka 2001, wastani wa ongezeko la malipo ya China kwa nchi nyingine kutokana na halimiliki ya kiujuzi ni asilimia 17 kwa mwaka, na mwaka jana malipo hayo yalifikia dola za kimarekani bilioni 28.6. China haikulazimisha mashirika ya kimataifa kutoa teknolojia zao ili kupata soko nchini China, na China imekuwa nchi inayoendelea ambayo imevutia uwekezaji kwa wingi zaidi duniani. Kusema kweli, China imepata faida kubwa kupitia ushirikiano wa kimataifa wa sayansi na teknolojia, lakini Marekani inapaswa kutambua kuwa ushirikiano huo unanufaisha pande zote. Mashirika mengi ya Marekani yanasema ongezeko la soko la China limesaidia kukabiliana na msukosuko wa fedha uliotokea mwaka 2008.

    Bw. Zhang amesema China itaendelea kufungua mlango zaidi na kusukuma mbele uvumbuzi. Kwa mujibu wa ahadi ilizotoa China wakati ilipojiunga na Shirika la Bishara Duniani WTO, imerekebisha vifungu zaidi ya 2,300 za sheria na nyaraka za serikali laki kadhaa. Kuanzia mwaka 2001 hadi 2017, wastani wa ongezeko la oda za China kwa bidhaa kutoka nje ni asilimia 13.5 kwa mwaka, na hivi sasa China ni nchi ya pili kwakuagiza bidhaa kutoka nchi za nje. Aidha, China inazingatia sana kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa sayansi na teknolojia. Katika siku za baadaye, binadamu watakabiliwa na mazingira magumu na changamoto mbalimbali, ushirikiano huo utakuwa na umuhimu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako