• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vita ya kibiashara inayochochewa na Marekani yaleta athari mbaya kwa biashara ya dunia

    (GMT+08:00) 2018-07-13 18:50:03

    Msemaji wa idara kuu ya forodha ya China Bw. Huang Songping leo hapa Beijing amesema, baada ya Marekani kuanzisha kutekeleza uamuzi wa kuongeza ushuru kwa baadhi ya bidhaa kutoka China, China pia imechukua hatua za kukabiliana na hali hiyo.

    Amesema kutokana na hali ya sasa, vita ya kibiashara inayochochewa na Marekani hakika italeta athari kwa biashara kati ya China na Marekani, na pia kuleta athari mbaya kwa biashara ya dunia.

    Takwimu iliyotolewa na idara kuu ya forodha ya China inaonyesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Marekani imezidi dola za kimarekani bilioni 288, ambayo ni ongezeko la asilimia 5.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo, na imechukua asilimia 13.7 kati ya thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji bidhaa za China kwa nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako