• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachuuzi Nairobi wataka wenzao kuachiwa huru

    (GMT+08:00) 2018-07-13 19:03:27

    Wachuuzi katika mji wa Nairobi wameitaka serikali ya kaunti ya Nairobi kuwaachilia huru wenzao sita ambao walikuwa wamekamatwa kwenye maandamano waliyofanya wiki hii. Wachuuzi hao walikuwa wameandamana kupinga kitendo cha askari wa kaunti ya Nairobi kuchukua hongo kutoka kwao kila mara.Hata hivyo uongozi wa Nairobi umesisitiza kuwa wachuuzi hao walivunja sheria za jiji nan i lazima wafikishwe kwenye mahakama ya jiji.Alhamisi wiki hii,wachuuzi walifanya maandamano makubwa na kuchoma matairi jambo ambalo lilipelekea maofisa wa polisi kuwarushia vitoa machozi. Shughuli za kibiashara pia ziliathiriwa pakubwa baada ya wafanya biashara wengi kufunga maduka yao wakihofia usalama wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako